Zari: Majizzo ni baba wa mtoto wa Hamisa sio Diamond
Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki wanajiuIiza maswali je Diamond ni baba halisi wa mtoto wa Hamisa?Ingawa Diamond amekataa tangu mwanzoni kuwa mtoto yule sio wa kwake licha ya Hamisa kumpa mtoto jina la baba ake na Diamond “Abdul Naseeb”.
Katika mahojiano aliyofanya Zari nchini Uganda amedai kuwa Diamond sio baba wa mtoto wa Hamisa na amekataa mara nyingi bali baba wa mtoto ni Majizzo, ambaye tayari ni baba wa mtoto wa hamisa, amedai kuwa sababu pekee inayomfanya majizzo akatae mtoto ni kwasababu anamuogopa Lulu Michael ambaye ni mpenzi wake, na pia amedai kuwa Majizzo ndiye anayemlipia kodi ya nyumba na kumuhudumia kila kitu. Lakini Zari amefunguka kuwa amekwisha mwambia Diamond kama mtoto atatokea akawa wake {za diamond} basi itabidi amuhudumie na amkubali ingawa hawezi kumlazimisha kama akikataa mwenyewe.
Diamond amekuwa akihusishwa kimapenzi na Hamisa kwa muda mrefu licha ya yeye kuendelea kukataa. Hamisa hajamuweka wazi mpaka sasa baba wa mtoto wake, licha ya kuwa kutangaza arobaini ya mtoto itakayofanyika hivi karibu ambapo bila shaka baba wa mtoto atajulikana.