Zari Azidi Kudidimiza Penzi La Diamond Platinumz

Image: Zari

Yawezekana inakuwa vigumu kwa mtu kutamka wazi  na moja kwa moja kuhusu kutokuwepo tena kwa mahusiano baina yake na mtu wa karibu aliyekuwa akimpenda, akimtangaz kwa watu na kujulikana na watu wote, saa zingine huwa ni maumivu kukubali hadharani kuwa ulimpenda mtu fulani lakini kwa sasa penzi lile limeisha.Hii inaweza pia kuwa ni moja ya sababu labda kwanini Diamond na Zari hawataki kuweka wazi juu ya kinachoendelea katika mahusiano yao.

Wakiwa kama wazazi wenye watoto wawili , ni vigumu kukubali ukweli kuwa inabidi kila mmoja aendelee na maisha yake, lakini vipo baadhi ya viashiria vinavoweza ku-Connect dots kuwa wawili hao kuwa hawapo katika mahusiano mazuri.

download latest music    

Zari the Bossy Lady, mzazi mwenzie na Diamond Platinumz amekuwa akipost picha na kuweka captions zeny maneneo ya kulenga kitu fulani kwa mtu fulani hata kama hasemi moja kwa moja kuwa  inamrenga nani zaidi.Ukimya wa watu hawa wawili na kutokuonekana pamoja pia kunafanya mashabiki kuamini kuwa penzi lao limekwisha.Katika moja ya post zake katika mtandao wa Snapchat jana , Zari The Bossy aliandika”ati nini ,?yule wa wawapi? hana gina ati mama T,unachako huku.Can i be left out of this drama plse.Naomba.” aliandika zari.

Hata hivyo , hivi karibuni ilikuwa Diamond alishereka sikikuu ya kuzaliwa kwake lakini mama mzazi wa watoto wake hakutokea wale kumtakia kheri ya sikikuu ya kuzaliwa.Hii bado haitoshi, Zari The Bossy Lady ameamua kufuta picha zote za Diamond katika ukurasa wake wa instagram, hali ambayo sio ya kawaida kwa watu wanaopendana kufuta picha gafla.lakini bado siku kama mbili zilizopita majina ya accounts za watoto wa Diamond katika instagram yalibadilika na kufutwa kwa jina la pili ambalo ni jina la baba yao mzazi Diamond Platinumz.

Kumekuwa na mambo mengi yanayoendelea kati ya watu hawa wawili ingwa bado hakuna aliyetayari kusema kwa uwazi zaid, hata hivyo vita hizi zilianza mara tu baada ya diamond paltinumz kukubali majukumu ya kuwa mtoto aliyezaliwa na Hamisa Mobeto ni wa kwake.Vita hii haijaisha na kila siku zinavyozidi ndivyo mambo mapya nayo yanazidi kuongezeka.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.