Zamaradi Adai Uvumilivu Ulimshinda Akaamua Kumwaga Povu Mtandaoni
Mtangazaji wa Wasafi Tv Zamaradi Mketema amefunguka baada ya bifu lake na mrembo Hamisa Mobetto na kudai uvumilivu ulimshinda ndio maana akamwaga povu lile Instagram.
Siku chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia kwenye vita kali ya maneno baada ya kugombana kisa nguo ambayo Zamaradi alivaa kwenye 40 ya mtoto wake.
Kwenye mahojiano na Bongo 5, Zamaradi amefunguka na kudai kuwa alifunguka na kuongea mambo Yale kwa sababu alishindwa kuvumilia kusemwa vitu vya uongo ili hali ukweli upo.
NI kweli nimeongea na kuweka vitu wazi lakini yule sio mimi ila kuna muda tu vitu vinakufika kooni na kushindwa kuvivumilia kwa sababu hata uongo unapozungumzwa sana hugeuka na kuonekana kama ndio ukweli na Watanzania ni watu wa kuchukua kitu kama kilivyo na kila mtu hongea lake na sikuongea kama ni povu bali nilitaka kuweka wazi ili watu waelewe nini kinaendelea”.