Z-Anto Afungukia Tetesi Za Kuoa Mke Wa Pili Kwa Siri
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Ally Mohamed maarufu kama Z- Anto ameibuka na kukana taarifa zinazosambaa kuwa ameoa mke wa pili bila kumtaarifu mke wake .
Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mwanamuziki huyo hivi karibuni alifunga ndoa na dada wa msanii wa filamu, Wastara Juma aitwaye Naima huku mke mkubwa akiwa hajui, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Dini ya Kiislamu.
Mke wa Z-Anto alisema alikuwa anakuta meseji kwenye simu ambazo mumewe huyo alikuwa akiwasiliana na huyo Naima akawa anamuuliza lakini anakuwa mkali, baadaye aligundua kuwa walishafunga ndoa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Z-Anto amekataa Tetesi Za kuoa mke mwingine na kusisitiza kuwa taarifa hizo zinazosambaa hazina ukweli wowote.
Niwaambie tu kwamba hizo habari za mimi kuoa hazina ukweli, mimi na mke wangu tuko vizuri kabisa hatuna tatizo ila kama anasema ameenda Bakwata mimi ndio kwanza nawasikia nyie.
Ningekuwa nimeoa ningeweka wazi tu lakini hakuna kitu kama hicho, kuhusu kuwa karibu na familia ya Wastara ni kwamba nilianza urafiki na familia hii kama miaka 10 iliyopita, nilikuwa namfanyia dua mume wa Wastara marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa anaumwa”.
Kuhusu picha zake na Naima za ndoa zilizosambaa kwenye mitandao, msanii huyo alisema kuna kitu walichokuwa wanakifanya kuhusiana na sanaa ambacho kwa sasa hawezi kukiweka wazi.