Young Killer Athibitisha Kuachana na Miss Hip-Hop
Mwaka 2016 msanii wa musiki bongo Young Killer wa Msodoki alitangaza kumuoa mwanamke aliyesema kuwa yuko nae katika mahusiano aliyekuwa akijulikana kama miss hip-hop, hali iliyofikia mpaka kumpachika jina ilo la miss hip-hop ikiwa kama ishara ya kuonyesha ni jinsi gani wamekuwa wakipendana.
Hata hivyo msanii huyo amefunguka hivi karibuni na kusema kuwa kwa sasa hayuko katika mahusiano ya kimapezni na mwanadada huyo tena kwaio maswala ya ndoa tayari yalishavunjika na hayupo katika mahusiano na miss hip hop kwa takribani miezi sita sasa ilikwisha pita.
kulikuwa na kutokuelewana kidogo kati yangu na yeye swala lilipopelekea tusiwe pamoja kwa takribani miezi sita sasa. -Aliongea Young Killer
Akiongezea kwa kufafanua zaidi msanii huyo amesema kuwa sio swala la usaliti hata kidogo lilowafanya waachane ila ni sababu za ndani ambazo hawezi kuziongelea zilizowafanya waachane.
Young Killer tangu alipotangaza yuko katika mahusiano na miss hip-hop , hajawahi kupata skendo yoyote ya kimapenzi na ndio maana hata walipoachana ilikuwa ni vigumu kujua kwa sababu ni moja ya wasanii waliaoamua kuweka mahusiano yao ya kimapenzi kuwa ni siri zao katika maisha.