Young Killer Arudisha Majeshi Kwa Miss Hip-Hop
Siku chache zilizopita msanii wa hip-hop nchini Young Killer alifunguka na kusema kuwa hana mahusiano tena na mpezni wake Miss hip-uop kutokana na kushindwa kuelewana kwao kuliowafanya washindwe kuwa pamoja kwa zaidi ya miezi sita.
hivi karibuni siku ya wanawake duniani katika snapchat ya msanii huyo ilionekana picha ya mwanadada huyo ambae alikuwa mpenzi wake na ikasemekana kuwa aliachana nae lakini inavyoonekana ni kwamba wawil hao wako pamoja tena.
Miss hip-hop na Young killer wamekuwa wapenzi kwa miaka mingi , lakini hapo katikati waligombana na kushindwa kukaa pamoja.