Wolper- Wanaume Wengi Wanatumia Wasanii Wa Kike Kwa Kiki
Muigizaji wa Bongo Movie na Mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper ameibuka na kudai ni ngumu kwa Mastaa wengi wa kike kupata wanaume wenye mapenzi ya dhati kwani wengi wao wanataka kuwa nao kwa ajili ya umaarufu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Wolper alisema kuwa mara nyingi wanaume wamewachukulia wasanii kama daraja la kusonga mbele au kukuza majina yao lakini siyo mapenzi ya dhati.
Ni hivi mastaa wengi hasa kwenye tasnia ya uigizaji wameamua kufanya maisha yao wenyewe na kusahau kabisa kama kuna jambo la kuolewa na ndiyo maana unaweza kukaa hata miaka mitano bila kusikia msanii wa kike ameolewa”.
Wolper amekuwa na Mahusiano na wanaume kadhaa ambao kiukweli aliwapa umaarufu wakati wa Mahusiano yao kati yao ni pamoja na staa wa Bongo fleva Harmonize ambaye alijizolea umaarufu sana alipokuwa na Wolper na muziki wake kukua.