Wolper Kuitangaza Tanzania Kupitia Mavazi
Msanii wa maigizo na ujasiamali nchini, Jackline Wolper anasema kuwa pamoja na kufanikiwa sana katika duka lake alilonalo la mavazi anatarajia kuanza kuitangaza tanzania kupitia kazi yake hiyo ya mavazi nje ya nchi.
Wolper ambae kwa sasa anamiliki duka la mavazi linalojulikana kama Wolper stylish anasema kuwa anashukuru kuona biashara yake sasa inafanya vizuri lakini pia anaona kuwa saa ndio muda wake wa kuanza kuitangaza baishara yake nje Tanzania.
Najivunia sana kazi ninayoifanya kwa sasa,imekuwa ikinizalishia wateja kila kukicha, imefika kipindi sasa natamani sana kufanya kazi nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda na kwingine ili niweze kuitangaza kupitia mavazi yangu ninayotengeneza.
Wolper anasema kuwa kipindi ananza biashara hiyo hakujuakabisa kama ataweza kufnaya biashara hiyo na kupata thamani kama ambavyo imekuwa ikimuingizia sasa, lakini kwa sasa anajipanga kuongeza kwanza maduka yake ya nguo nje ya Dar Es Salam ili kuwapatia pia wateja wake wa mikoani huduma yake.