Wema Sepetu- Nina Kitu Cha Ziada Ambacho Wengine Hawana
Muigizaji wa Bongo movie Madam Wema Sepetu ameibuka tena katika jitihada za kulitetea Jina lake la Tanzania Sweetheart na kusema ana kitu ambacho wengine hawana.
Kwa wiki kadhaa sasa Wema amekuwa Kwenye vita kali katika harakati za kutetea Jina lake la Tanzania Sweetheart ambapo hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashabiki kudai hana vigezo vya Jina hilo Tena na kutaka Hamisa kuwa Tanzania Sweetheart.
Kwenye mahojiano yake na gazeti la Risasi Jumamosi, Wema amesema hawezi kustaafu kutumia jina hilo kwa sababu wakati anapewa na mashabiki wake wa jijini Arusha, hakuambiwa kama kuna kustaafu hivyo jina hilo ni lake na ataendelea kulitumia.
Kwani kuna kustaafu? Sasa nani mwingine atumie jina hilo wakati Tanzania Sweetheart ni mmoja tu? Kwanza akianza kulitumia mtu mwingine mashabiki watakubali? Kila kitu kinaenda na mazoea, watu wamenizoea mimi na nitabaki kuwa mimi tu na hakuna kama mimi“.