Wema Sepetu Kwenda Nairobi Kwa Ajili Ya Tundu Lissu
Akiwa kama mmoja wa watu walikuwa mstari wa mbele sana katika kufanya kampeni katika mitandao ya kijamii ili kuchangia ela za matibabu kwa ajili ya mbunge wa Singida kupitia chama cha upinzani Chadema, mwanadada mrembo na anaependwa na watu Wema Sepetu aonyesha wazi hisia zake za furaha baada ya mwanaharakati huyo kutoka ICU.
Tundu Lissu ambae alikuwa ICU kwa muda wa takribani mwezi sasa tangu iliporipotiwa kuwa hali yake ni mbaya baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana alipokuwa nyumbani kwake Dodoma na kuhamishwa kwa matibabu nchi Kenya, jana kwa mara ya kwanza ameweza Kuongea na wananchi wanaomsapoti na kuonyesha kuwa yeye anaendelea vizuri.
Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu wengi maarufu walioonyesha jinsi gani wamefurahishwa na hali ya mbunge huyo kutengemaa na amehaidi kupanga safari ya kwenda Nairobi kwa ajili ya kwenda kumjulia hali mbunge huyo huku akisema kuwa alikuwa anaogopa kwa muda mrefu kwenda kumuona kwa sababu hasingeweza kuvumilia kumwangalia akiwa na yale maumivu kitandani kama ilivyokuwa ikiripotiwa na watu wa karibu waliokuwa na mgonjwa huyo hospitali kuwa hali yake ilikuwa ni mbaya.
Katika ukurasa wake wa instagram , Tanzanian sweetheart aliandika”What doesn’t kills you always makes you stronger,and you will come baq stronger than you have ever been, Our True Leader…our Hero..sasa naweza andaaa safari ya Nairobi kuja kukuona …. I couldn’t bare to see you in pain…This picture just melted my heart…..God sure is Good…All the time #ATrueLeader#OurOnlyHope#OurHero#SuperMan” aliandika Wema Sepetu
Taaarifa za kuendelea vizuri kwa mwanaharakati huyo zimegusa watu wengi kwa namna tofauti huku wengine wakizidi kumuombea ilia aendele kupona haraka, hata hivyo Wema bado anafanya kampeni za fedha za matibabu kwa sababu bado kuna pesa zinahitajika ili kuendeleza matibabu ya mbunge huyo.
Ikumbukwe kwamba Wema alipoamua kuingia katika siasa alikuwa ni mmoja wa wasanii waliokuwa wakiisapoti Chama Cha Mapinduzi lakini hivi karibuni Wema Sepetu aliamua kubadilisha msimamo wake na kubadilsh upepo na kuingia Chadema.