Wema Sepetu Hatafuti Kiki Kwa Matukio Anayofanya Ndio Maisha Yake – Martin Kadinda
Mwanamitindo na mbunifu wa mavazi Martin Kadinda, amefunguka na kudai kuwa matukio yote anayofanya Wema Sepetu na kutengeneza headlines sio kwamba anayapanga ili kupata kiki bali ndio maisha yake halisi.
Martin Kadinda aliyekuwa meneja wa msanii wa filamu za bongo movie, Wema Sepetu amefunguka na kukiri kuwa matukio mengi anayofanya Wema sio katika jitihada za kutafuta kiki kama watu wengi wanavyodhani bali ndio maisha yake halisi.
Miezi hii michache Wema amekuwa akitawala sana vichwa vya habari kuanzia kuhama hama chama kutoka CCM kwenda Chadema kisha kurudi tena CCM na picha za kimahaba na mpenzi wake kuwekwa kwenye vichwa vya habari yaani ni kila siku Wema haishiwi na drama hadi kufikia hatu ya watu kudai kuwa anajitengenezea kiki kimaksudi ili aandikwe kwenye magazeti na kuongelewa kwenye mitandao ya kijamii.
Martin amekataa tuhuma hizo za Wema kupenda kiki na kufunguka mambo haya kuhusu maisha ya Wema alipokuwa anahojiwa na Bongo 5:
Wema Sepetu ni Wema bila hiyo mitikisiko ya kuongelewa sio Wema unaweza ukaona hapa katikati nilimwambia atulie lakini mashabiki zake wanaanza kuuliza Wema vipi mbona kimya yaani unaona watu wanamiss na kitu ambacho wengi hawajui Wema hatengenezi matukio ni mtu anayeishi maisha yake anafanya kitu anachotaka kufanya na hajali watu wengine wanasema nini kuhusu yeye”.
Kwenye mahojiano hayo Martin Kadinda alipotakiwa amshauri Wema jambo lolote alikiri kuwa hawezi kumshauri tena kuhusu jambo lolote kwenye media kwani tayari amesha mshauri sana.