Wema Sepetu Apata Dili Nono, ni Baada ya Kuonekana SZIFF
Msanii wema septu ambae aliingia katika headline wiki hii baada ya kupokea tuzo za sinema zetu kupitia filamu yake ya heaven senr amepata dili nono na kusaini =mkataba na kampuni moja ya kusambaza filamu zake inayojulikana kama Auguster.
Mkataba huo umesainiwa leo katika ofisi za Azam Tv na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwepo mwandishi na mtayarishaji na rafiki wa karibu wa star huyo Neema Ndepanya.
Wema anasema kuwa tangu kutolewa kwa movie hiyo mashabiki wake walikuwa wakiipata movie hiyo kupitia applicatuon yake tu na hakukuwa na DVD za filamu hiyo lakini sasa hivi wataanza kuipata kupitia huko.
Wema anasema kuwa uamuzi wa kampuni hii kusaini nae mkataba unakuja pale ambapo filamu hiyo imeweza kupata tuzo mbili hivyo kuonekana ni moja ya filamu bora pia.