Wema Sepetu Akanusha Ndoa na Diamond Platinumz.

Siku ya wanawake duniani kuna habari ili-trend sana katika mitandao ya kijamii baada ya msanii Diamond kutangaza kuwa kabla mwaka huu haujaisha basi ni lazima atakamilisha swala la kuoa.jambo ambalo ni la kheri sana lakini swala likaja kwamba  je Diamond anataka kumona nani kati ya wanawak wote aliokuwa nao katika mahusiano ilhali ameshagombana na mama mzazi wa watoto wake.

Wengine walipata jibu la haraka kuwa lazima atakuwa ni wema sepetu kwa sababu kwa sasa mwanadada huyo yupo karibu sana na Diamond licha ya kwamba mara ya kwanza walikuwa maadui, lakini pia wawili hao wanategemea kuanza kufanya kazi katika jengo moja kwa kuzingatia kuwa Wema atakuwa na kipindi chake Wasafi Media.

download latest music    

Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa katika usiku wa Vikings katika ukumbi wa Kings Solomon  kuhusu swala hilo Wema Sepetu amekanusha kabisa tetesi hizo na kusema kuwa swala la yeye kuolewa na diamond halipo na halitakuja kutokea hata mara moja .

nataka kugunga ndoa lini, na nani? whatever it is trending sio kweli kuhusu mimi na kwa upande wangu ninasema kabisa hicho kitu hakiwezi kutokea kabisa, so everything is trending sio kweli kabisa.- Aliongea Wema akionekana mwenye kuhamaki.

Kitendawili hiki kinazidi kuwa kikubwa kwa sababu mwanamuziki diamond ametangaza ndoa bila kusema rasmi ni mwanamke gani atakae funga nae ndo kwa sababu baada ya kugombana na mama wa watoto wake msanii huyo ameazna kujiweka katika hali ya amani na wanawake zake wote aliowahi kutembea nao ikiwemo Wema Sepetu hata Hamisa ambae wamekubaliana kumlea mtoto wao kwa amani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.