Wema Sepetu Ajuta Kuchora Tatoo
Msanii wa bongo movie ambae haishi kusema kwenye mitandao kila siku Madame Sema sepetu amefunguka na kusema kuwa katika vitu anavyochukia katika mwili wake ni tatoo kubwa aliwahi kuichora maeneo ya shingoni.
Wema Sepetu anasema kuwa hiyo ni moja ya tatoo zake za mwanzo kabisa alizowahi kuchora na wakati anachora hakuwa anafikiria kitu sana lakini tatoo hiyo iliyopo shingoni ni kubwa kuliko na imekuwa ikimkera sana kwa sasa.Hata huvyo Wema anasema kuwa tatoo iyo ambayo imetapakaa shingoni waktai anachora alimwambia mchoraji achore na iyonekane shingoni hivyo mchoraji aliamua kuchora umbo kama la mjusi anatamani kuifuta lakini anaogopa maana anaambiwa kufuta tatoo kunasababisha maumivu sana.
“Natamani sana kuifuta tatoo hii ila nasikia vibaya na pia niliambiwa kufuta tatoo inaumwa sana, lakini ingekuwa uwezo wangu wala hata isingekuwepo mpaka sasa” alisema Wema Sepetu
Ukiachana na tatoo iliyopo shingoni ambayo madame wema sepetu anataka kuifuta, wema ni mmoja wa watu wenye tatoo nyingi sana katika mwili wake na zimekuwa zikiongezeka kila leo.
Watu wengi sana wamezua tabia ya kuchora michoro ya tatoo mwilini , baadhi yao uchora michoro ya tatoo za majina ya watu wao wa karibu au watu wanaowapenda. Ingawa pia inaweza kuleta shida pale wale watu wanaowapenda wanapokuwa wamegombana nao au kuitilafiana wengi ujikuta wakiangaika kuziondoa na kuishia kuchora michoro ya maua au michoro isiyo eleweka.
Ikiwa ni kama moja ya urembo mwilini tatoo inaweza kuchora ya muda mfupi kulingana na mahitaji yako, inasemekana kuwa kuchora tatoo ya moja kwa moja kwenye ngozi uweza kusababisha kansa ya ngozi, hivyo kwa urembo wanaohitaji wanapaswa kufikiria njia mbadala zaidi ya hiyo, lakini pia inakuwa shida pale unapotaka kuiondoa.