Wema Aweka Ahadi Nzito kwa Rc Makonda.
Msanii Wema Sepetu amejibu kwa kishindo cha kuweka ahadi pongezi kubwa aliyopewa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda baada ya siku ya jana Mh huyo kumpongeza Wema kwa kushinda tuzo za sinema zetu kupitia filamu yake ya heaven sent.
Wema amemshukuru sana makonda kwa kumtia moyo na kumfariji sana kwa kipindi hiki ambacho anahitaji sana kuwa anafarijika ili kufanya vizuri zaidi.
‘lakini pia naomba nikuahidi sitakuangusha ,maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa”
Wema pia anaendelea kwa kusema kuwa katika tasnia hiyo ya filamu kwa sasa wanataka watu wanaojielewa na wanaotaka kufanya kazi na sio watu wanaokurupuka na kuongea mambo bila kudadavua.
Yote yanawezekana , wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana,najivunia kuwa mmoja kati yaonajua hata wewe unajivunia sana kuwa kati yetu sisi,ukiwa kama mlezi na kutuongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na inshallha tutafika.”