Wema Akiri Kutomsahau Idriss Sultani Kamwe.
Mwanadada ambae kila kukicha anakuwa na jipya kwa mashabiki wake Wema Sepetu, siku ya jana aliwashangaza mashabiki wake baada ya kuweka picha ikimuonyesha yupo na Idrsis Sultani na kukiri kuwa mwanaume huyo ni moja ya wanaume walioweza kuweka historia kubwa katika maisha yake kwa Vile alivyowahi kumfanyia ambavyo hatokaa hazisahahu kamwe.
Ikiwa jana ni siku ya kuzaliwa ya mwanamitindo na mchekeshaji huyo ambae pia aliwahi kuwa mshindi wa Big Brother miaka iliyopita, Wema Sepetu aliamua kufichua hisia zake kwa kumtakia kheri ya sikukuu hiyo ya kuzaliwa kwa idris na kuandika hivi”happy birthday to this special being..so many things you have done that left mark in my life, God keep you well-being..”
Katika kipindi chao cha mapenzi Wema Sepetu na Idris Sultani , Wema alipata mimba na kutangaza hadharani kuwa walikuwa wakitegemea watoto mapacha lakini kwa bahati mbaya siku chache tangu kutangazwa kwa mimba hiyo ilitoka na kuacha alama kubwa ya maumivu kwa Wema Sepetu.
Penzi la Idriss na Wema lilidumu kwa muda kidogo na ndipo walipoachana huku kila mmoja akikataa kusema sababu ya ugomvi wao.
Hata hivyo sio kwa Wema tu , hata Idris amekuwa akikiri kuwa Wema Sepetu ni maoja kati ya wanawake aliowahi kuwa nao katika mahusiano na hatokaa hamsahau kutokana na mda mzuri aliokuwa nao walipokuwa wote.