Wazazi wa Nandy ni Zaidi ya Marafiki
Wazazi wa mwanadada Nandy leo wametinga mjengoi clouds tv katika kipindi cha clouds 360 huku lengo lao kubwa ikiwa ni kutaka kutambulisha wimbo mpya wa mtoto wao ambapo yeye ameshindwa kuhudhuria kwa sababu ya kutokuwepo nchni.
Wazazi wa mwanadada huyo wamekuwa wakimsapoti sana mtoto huyo karibia kwa kila kitu na hata kazi zake zimekuwa zikieda sawa kutokana na sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa wazazi wake.
Nandy ambae amekuwa hata akitumiwazazi wake kama model katika baadhi ya nyimbo zake amekuwa pia akioenekana kuwa karibu sana na baba yake mzazi kutokana na mapenzi yanayoonekana katika mitandao ya kijamii.
Wazazi hao ambao hivi karibuni walikabidhiwa nyumba mpya na mtoto wao huyo wa kike kutokana na mafanikio yake katika muziki anasema kuwa wamekuwa na furaha siku zote kutokana na mafanikio ya binti yao.