Wastara- Maisha Yangu Bila Sajuki Yanakuwa Magumu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Wastara Juma maarufu kama ‘Wastara Sajuki’ amefunguka na kuongelea changamoto anazopitia tangu Sajuki afariki.

Wastara na Sajuki walishangaza watu wengi baada ya kufunga ndoa hata baada ya Wastara kupata ajali ya gari na kukatwa mguu lakini Sajuki bado alikuwa Wastara.

download latest music    

Kwa kipindi kirefu sasa Wastara amekuwa akipitia wakati mgumu na maradhi yake ya mguu ambapo ni juzi juzi tu aliomba msaada wa kuchangiwa pesa kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India lakini alisindikizwa na tuhuma kibao za utapeli.

Kwenye mahojiano aliyofanya kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Wastara amefunguka na kusema hivi sasa anapiga wakati mgumu kwa ajili ya Sajuki anatamani angekuwepo naye:

Sajuki ananipa wakati mgumu sana kwenye maisha yangu, alikuwa na nafasi kubwa kwangu, kwenye utendaji wa kazi, pili alikuwa ana jukumu kubwa la kumuangalia Wastara, nilikuwa kama mtoto wake, mimi nilikuwa fighter sana kwenye familia yangu, hivyo alihakikkisha siumizwi na lolote, hayupo tena mtu wa namna hii sasa hivi kwenye maisha yangu, naweza nikatetea wenzangu lakini nikiumizwa mimi sina wa kunitetea, lakini yeye alikuwa anacover nafasi zote, anahakikisha mke wangu haumizwi na kitu chochote“.

Wastara pia amefanya mkutano na waandishi wa habari kwani amedai anaenda nchini Sweden kwa ajili kuhudhuria Kongamano la wasichana wanaolewa ndoa za utotoni ambapo yeye ni balozi kwani ndoa yake ya kwanza alikuwa na miaka 13.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.