Wastara Atafuta Mbinu Mpya Kwa Ajili Ya Kusaidia Wamama na Watoto
Muigizaji wa Bongo movie mwanamama Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajukia amefunguka na kusema amekuja na project mpya ambayo imejikita katika kuhakikisha inatoa msaada kwa wamama na watoto.
Wastara ameweka wazi kuwa kupitia priject hii ataweza kutimiza ndoto yake ya kusaidia jamii aliyokuwa akiiota kila siku.
Kwenye mahojiano yake na Risasi Jumamosi, Wastara alisema yeye kama kioo cha jamii na mambo aliyopitia kwenye maisha, ameamua kuanzisha mradi huo alioupa jina Anzia Hapa Wastara akiwa na nia ya kuwasaidia akina mama na watoto.
Kama unavyojua, mbali na kuwa msanii, mimi ni Balozi wa Wanawake Afrika kupitia Shirika la Wanawake na Watoto la Sweden (Asovu). Nimeamua kutimiza ndoto yangu ya kusaidia watoto na wanawake, pia kwa kupitia chama hicho ambapo rasmi nitakizindua Jumamosi (leo)”.
Wastara ameweka wazi kuwa kwa Kupitia project hii basi anaamini atasaidia wanawake na watoto wengi ambao nao wanahitaji msaada kama yeye na kusaidiwa na Watanzania wenzake.