Wasanii Waguswa na Kijana Aliyeibuliwa na Ugonjwa wa Kutisha
kuna baadhi ya picha na video zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha mtoto wa kiume aliyekonda sana na kudhohofika kiasi kwamba anahitaji msaada wa kila kitu,
Mtoto huyo aliibuliwa na mwanadada floraj lauwo kutoka mwanza, huku akiomba watanzania wamsaidie ili aweze kupata pesa kwa ajili a matibabu yake nje ya nchi na kuisaidia familia yake kwa ajili ya kupata chakula bora na malezi mazuri kwa kipindi hiki anachoumwa.
Watu wengi wameguswa lakini jamii inazidi kuwashukuru wasanii ambao wanamajina katika jamii kwa kuliona hili na kulitolea msaada kwa sababu hii imefanya watu wengine pia waguswe kupita wao.
Wasanii kama Wema Sepetu, Zari the Bossy, Riyama Ally, mwanadada Zamaradi Mketema, kaka Millard Ayo,Dogo janja na wengine wengi ambao waliweza hata kuhamasisha kupitia kurasa zao .