Wasanii Wa Bongo Movies Watakiwa Kujiandikisha Kumuona Ramsey Nouah

Wiki iliyopita msanii mkubwa kutoka nchini nigeria Ramsey Nouah alikuja Tanzania , ambapo alipokelewa na kuongozwa kufanya  baadhi ya shughuli na mwanadada mjasiriamali na mrembo Jokate M, baada ya hapo msanii huyo alipata nafasi ya kutembelea kaburi la msanii mkongwe na aliyekuza tasnia ya muvi za Tanzania Steven Kanumba akisindikizwa na wadau wa filamu na familia ya marehemu.

Lakini hivi karibuni hasa jana, kulizuka kwa mtafaruko katika mtandao wa kijamii baada ya kutoka kwa tangazo kutoka kwenye ujumbe wa msanii huyo wakidai kuwa Ramsey alitaka kuongea na wasanii wa bongo movies lakini kwa yoyote mwenye kutaka kuongea nae basi ni lazima kujiandikisha ndio aweze kuonana  na msanii huyo.

download latest music    

Tamko hili lilionekana kuwakwaza baadhi ya watu kwa sababu kwa maoni yao ni kwamba  hii inashusha hadhi ya wasanii wa Tanzania hasa wa maigizo kwa sababu akiwa kama msanii mkubwa hata Tanzania pia kuna wasanii wakubwa kama yeye hata kama hawajajulikana sana kimataifa kaka yeye, haikuwa na haja ya ramsey na ujumbe wake kutaka kuongea na wasanii wa Tanzania kwa style ya kuandikishana majina kama walivyotaka wao.

Hii ilionyesha ni kama kuna dharau flani inataka kutokea kwa wasanii wakubwa wa Tanzania kwa sababu hata kama msanii huyo mkubwa wa Afrika alitaka kuisaidia tasnia hii basi waliopswa kujiandikisha ni wale wasanii wachanga ambao wanataka kujifunza kitu kutoka kwake lakini kwa wasanii wakongwe na wakubwa kama kina Single Mtambalike, Jb,Ray na wakina Wema hii ilikuwa ni fursa ya wasanii wakubwa Tanzania kukutana na msanii mwenzao mkubwa kutoka Nigeria na si vinginevyo.

Hata hivo tangazo hilo ambalo lilionekana katika ukurasa wa Jokate Mwegelo lilifutwa muda mfupi baada ya kuwekwa, mashabiki na baadhi ya wadau wa sanaa walisema hii ni dharau kwa wasanii wakubwa tanzania lakini pia inasmekana kuwa kuna interest anayoipata msanii huyo kutoka nigeria endapo atapata list ya wasanii wakubwa waliojiandikisha kwa ajili tu ya kumuona yeye,hii ni moja ya jumbe zilizosambaa zikijaribu ku-justify kitendo hicho.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.