Wakina Mama Bongo Muvi Waanzia Mashuleni, Ni Kuhusu Elimu Ya Ushoga
Wana mama kutoka Bongo movies kupitia katika foundation yao inayojulikana kama Malezi Daima Foundation wameungana na kuanza kutoa elimu mashuleni hasa katika shule za sekondari huku elimu yao ikijikita kuwafunza wanafunzi wa kike na wa kiume kuhusu usahgaji na ushoga na athari zake.
Bi Sonia ambae ni mwenyekiti wa foundation hiyo amesema kuwa wazazi hao wameona ni bora kujitolea kuzunguka katika mashule mbalimbali ili kuwasaidia watoto ambao wanakutana na vishawishi vingi na kujikuta wakiingia katika tabia hizo.
Bi Sonia mbele ya wanafunzi.
Kama wamama wa bongo muvi tumeona ni bora tuungane na kutoa hii elimu mashuleni ili kuwanusuru na mimba za utotoni, ndoa za utotoni, magonjwa ya ajabu,matumizi ya madawa ya kulevya, usagaji na ushoga pia kuondokana na malezi mabaya nje na ndani ya shule .hadi sasa tumeshatembea shule kama tano hivi dar na mikoani pia.lengo letu ni kuwapa watoto malezi mazuri ambayo kama wanayakosa nyumbani basi wayapate shuleni.
Wamama wa bongo muvi wanaounda foundation hiyo ni pamoja na Bi Sandra, Natasha,Asha Boko, Herieth Chumillah, Grace Mapunda,Daina Njaidi, Mama Teckla Mjata,Mama Nyamayao na wengine wengi.
Wamama kutoka Bongo movies wakiongea na wanafunzi wa shule ya sekondaro buza jijini dar es salaam.
Bi. staa akitoa zawadi kwa wanafunzi.