Wadukuzi Wamliza Aika wa Navy Kenzo
Mwanadada kutoka katika kundi la Navy kenzo, Aikah amejikuta analizwa na wadukuzi wa mitandao baada ya akaunti yake ya instagram kuibiwa na wabbobezi wa mambo na kumfanya ashindwe kuwa na access na akaunti hiyo kwa zaidi ya masaa sasa.
Hata hivyo mwanadada huyo ameomba mashabiki zake kuwa na subira ili aweze kulishughulikia swala hilo huku akiwataka wasije kudanganywa na kujikuta wakitapeliwa kupitia jina lake.
Swala la wasanii kuibiwa kaunti zao katika mtandao wa instagram imekuwa swala la kawaida huku ikishndikana kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwa sababu msanii na kosa baadhi ya mambo hasa anapokuwa anashindwa kuwa karibu na akaunti hiyo kwa muda