Viongozi Wa Dini Wamjia Juu Diamond
Katika wimbo wake mpya ambao Diamond Platinumz ameimba unaojulikana kwa jina la Hallelujah, baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wameibuka na kuzungumzia swala hilo na kusema kuwa Diamond hajafanya vizuri kuimba wimbo huo kwa sababu huku ni kama kukiuka imani yake ya kiislamu na kumsujudia nabii Issa, lakini pia katika wimbo huo diamond alionekana kuvaa cheni zenye msalaba ikimaanisha anakubali kuwa kiongozi huyo wa dini alisulubiwa msalabani.
Kitendo cha kuvaaa msalaba kilichoonyeshwa na Diamondni ishara ya yeye kuonyesha kuwa anakubali kuwa nabii issa kasulubiwa, sasa si bora hatuambie kuwa yeye sio muislamu, kwanini uwaambie watu kuwa wewe ni muislamu alafu unavaaa msalaba, na katika nyimbo zake si bora angeimba nimbo nyinyine nyingine tu, anaimba Halleluyah” aliongea shekhe kipozeo
Halleluyah ni moja ya nyimbo mpya za Diamond ambazo zinafanya vizuri duniani kote, wimbo huo uliotoka mwezi uliopita amewashirikisha kundi la muziki la MorganHeritage .Ikiwa kama nyimbo mojawapo iliyomfanya Diamond aendele kujulikana kimataifa na anaona alipiga hatua kubwa katika muziki kutokana na kushirikiana na wanamuziki wakubwa Duniani, Diamond aliimba wimbo huo kwa dhumuni la kikidhi mahitaji ya mashabiki.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa msanii Diamond na wasanii wengine kuongelewa na viongozi wa dini zao kutokana na nyimbo wanazoimba, lakini kwa upande wa Diamond haijawa wazi kuwa mambo hayo yote ambayo Diamond amefanya katika wimbo huo alimaanisha kile ambacho viongozi wa dini watakuwa wamekimahanisha pia.
Bado diamond hajajibu chochote kuhusu tuhuma hizo alizoshtakiwa na viongozi wa dini yake, lakini nadhani inampasa kujibu ili aweze kuweka wazi kwa watu pia, sio tu katika wimbo huu tu , lakini pia baada ya wimbo wa Eneka kutoka kuna baadhi ya mashabiki zake ambao waliongelea swala ya msanii huyo kuoneka akiwa amevaa cheni yenye msalaba inayoashiria ishara tofauti na dini yake, lakini pia kuna badahi ya alama ambazo mashabiki wake walihoji Diamond kuzionyesha zilizokuwa na walakini,