Vijana Mbeya Wamlilia Masogange, Waelezea Alivyokuwa Akiishi na Watu.
Vijana na watu mbalimbali kutoka Mbeya wamefunguka na kusema kuwa msiba wa mwanadada Agness umewagusa sana kwa sababu pamoja na kwamba Agness alikuwa akiishi Jijini Dar lakini alikuwa ni moja ya watu waliokuwa hawajitengi na familia yake kwa sababu mara nyngi alikuwa akifika mpaka nyumbani na alikuwa akisaidia wengine.
Wakiongea kwa njia ya simu vijana hao waliokuwa live katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv kupitia simu ya mwanadada Shiloleh , vijana wengi waliokuwa katika msiba huo ambao wanafanya kazi ya boda boda wanasema kuwa Agness alikuwa siku zote anashirikiana na wenzake na alikuwa na upendo sana na watu wa mtaani,
Vijana hao wanasema kuwa kwao Agness alikuwa ni kijana wa kuigwa kwa sababu alitumia fursa na kipaji chake kuikwamua familia yake lakini pia hata bada ya kupata mafanikio hakuweza kuwadharau wengine kwa sababu aliamini kuwa kule ndipo alipouwepo na ndipo alipokulia,
Mpaka asubui hii walipokuwa wakiongea na shiloleh aliyekuwepo nyumbani kwa baba wa marehemu, gari la maiti na watu waliosindikiza mziba huo kutoka Dar , wansema kuwa bado hawajafika kijijini kwao mbalizi lakini wanategemea kuzika leo mchana kwa sababu wanategemea kuipokea maiti hiyo asubui hii.