Vannesa ni Kila Kitu Katika Maisha Yangu:-Jux
Mwanamuziki wa RnB Jux ameshindwa kujizuia na kujikuta akisema kuwa kwa mafanikio aliyonayo sasa hawezi kuacha kumsema vannesa kama mtu ambae amekuwa akimsapoti katika kazi hizo na ndio maana kwa sasa amekuwa akisonga mbele zaidi katika muziki.
Jux anasema kuwa tangu amekuta na vanesa maisha yake na muziki wake umekuwa ukibadilika na ndio maana hashindwi kusema kuwa vanesa ni kila kitu kwake kwa sasa.
kwakweli siwei kuacha kumshukuru mungu kwa sababu ya kipaji changu nilichozaliwa nacho, lakini pia nawashukuru wazazi wangu kwa sapoti kubwa abayo wamekuwa wakinionyesha na kunipa katika muziki wangu lakini pia mpenzi wangu Vee Money amekuwa mtu muhimu sana kwangu, yeye ni kla kitu kwangu katika maisha yangu na muziki wangu.
Aliyasema hayo Jux alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa siku chache zilizopita.