Vanessa Mdee Afunguka Baada Ya Kuimba Nyimbo Ya Kihindi
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ameibuka na kuanika ugumu alioupata baada ya kuandika na kuomba wimbo wake wa Kihindi unaoitwa ‘Vaishnav Jan’.
Katika mahojiano yake na Risasi Vibes, Vanessa amedai kuwa alifuatwa na ubalozi wa India ambao upo Tanzania ili autunge na kuuimba wimbo huo kwa ajili ya kutumika kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya kufariki kwa baba yao wa Taifa, Mahatma Gandhi ambayo hufanyika kila mwezi Oktoba huko India.
Orijino wa wimbo huu umefanywa na msanii wa kwao wa zamani sana wa kike, sasa katika kuadhimisha miaka hiyo 150 wakaona watafute mtu mbadala wa kufanya kava kwa ajili ya kucheza pamoja na video ndipo wakanipata mimi,” alisema Vee Money na kuongeza“.
Kwa hiyo kutokana na fursa hiyo nikafanya wimbo nikiongoza na mwalimu wa lugha ya Kihindi na tukashuti video ndogo ambayo ipo Youtube. Ilikuwa kazi kwani Kihindi sijui lolote hata ukinitukana lakini kwenye kuimba nimefanya vizuri na tayari nimepokea barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje India, Swaraj akinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya“.
Baada ya kuimba wimbo huo serikali ya India ilimtumia barua ya shukrani na kuonyesha kufurahishwa na wimbo ule.