Uzuri Unaendana na Kufanya Kazi Kwa Bidii-Poshy Queen
Mrembo aliyejizolea umaarufu kwenye Mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata Jackline Obeid maarufu kama Poshy Queen amefunguka na kutoa siri ya kuogopwa na wanaume.
Poshy Queen ameibuka na kudai kuwa siri pekee ya mwanamke kuogopwa na wanaume ni kufanya kazi ili kuweza kusimama mwenyewe na hasa kuweza kujitegemea.
Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Poshy Queen, amesema kuwa staa yeyote akiwa mzuri halafu akafanya kazi anazidi kung’ara na hata wanaume wanamugopa wanajua wazi kwamba, si mwanamke wa mchezomchezo.
Unapokuwa staa na ukaamua kufanya kazi basi itakuwa dawa moja kubwa sana ya kukulinda na wanaume, lazima watakuogopa; utaheshimika na kisha uzuri wako utaonekana mara dufu”.