Uwoya: Nimetafuta Mwanaume Wa Umri Wangu Sio Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Irene Uwoya ametoa kauli ambayo imethibitisha kuachana  kwake na mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Kwa mwezi sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya ameachana na Dogo huku tetesi hizo zikichangiwa na Safari aliyoifanya Uwoya wiki chache zilizopita nchini Dubai ambako ilisemekana alikuwa na mwanaume mwingine.

download latest music    

Ingawa wawili hao walishawahi kukataa tetesi za kuachana Lakini sasa inaonekana kama wameamua kuweka mambo hadharani kwani Uwoya ameandika maneno ambayo yameleta sintofahamu.

Kupitia page yake ya instagram, Uwoya ameweka comment kwa shabiki mmoja aliyemhoji Kuhusu Dogo Janja ambapo ameandika kuwa ameamua kumuacha Dogo Janja na kutafuta mwanaume anayeendana naye kiumri.

Irene Uwoya aliandika maneno  haya:

Simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? Sasa nimefata ushauri jamani…..au keshakuwa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.