Uwoya Awatolea Povu Wanaosema Kuhusu Mali Zake
Mwanadad Irene uwoya ameamua kuwajibu watu waliokuwa wakizusha baadhi ya maneno kuhusu mahusiano yake ya sasa huku tetesi zikidai kuwa mwanadada huyo kwa sasa yuko katika mahusiano na kigogo mmoja anaefanya kazi katika serikali ya kenya.
Maneno ya mashabiki yamekuwa mengi kutokana na kuwa mwanadada huyo amekuwa akioneana akila bata non stop katika viwanja mablimbali huku akionyesha jeuri ya pesa katika kurasa zake za mitandao.
Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa watu wamekuwa wakiangaika sana kufatilia maisha yake na kusema mara anatoka na huyu mara yule lakini hakuna mwenye ukweli zaidi ya yeye mwenyewe hivyo waache kumfatilia.
mhhhh bongo jamani, mara natembea na john mara na musa , mara uritho mara mafao ya baba yake, mara hana lolote kwakweli kazi mnayo na ndio maana hamna kazi za kufanya jua likisogea na nyie mnasogea.daaah ..poleni sana kifupi tu ni kwamba mnajisumbua sana fanyeni maisha yenu….