Usiruhusu Marafiki Kuingia Mahusiano Yako.
Sio kila aliye karibu ykao atakuwa mkweli kwako kwa kila kitu, mahusiano yako ya mapenzi inafiak sehemu inabidi yabaki kuwa ya peke yako.Unaweza kukumbwa na matatizo ya kiuitaji msaada na ushauri , lakini hii haimaanishi kuwa anapaswa kutawala hadi maamuzi yako pia.Hizi ndio njia zinazoweza kukufanya marafiki zako wasiingilie mahusiano yako na mpnzi wako.
1.Uthibiti wa taarifa zako za mahusiano
kadri unavyokuwa wazi kuhusu taarifa zako za mahusiano ndivyo unavyfnaya watu watake kuendelea kujua nini kinaendelea kwako,pia hii itawafanya wawe huru kutua maoni yao kwako na kudhani kuwa wanadhaman ya kila kitu chako.Hivyo kama unapata matatizo juu ya mapenzi ni bora kukaa muda mrefu kutafakari juu ya hilo, soma vitabu na angalia makala zinazohusu mahusiano.
2.Kuwa na upekee wa mambo
Kuna tabia uwa ni za kipekee toka kwa mwenzi wako, hivyo unaweza ukaomba ushauri ukihisi kuwa ushauri wa rafiki zako uanweza kutatua tatizo ilo kumbe mawazo unayoyabeba na kutaka kuyafanyia kazi hayaendani kabisa na tabia za mwenzi wako au tatito mlilonalo na mtu wako, hii inaweza kukuumiza zaidi au hata kuaribu mahusiano kwa kuiga kitu kisichoendana na mahusiano yenu.Jifunze kufanikisha mahusiano yenu kwa kutumia njia zako mwenyewe.
3.Muamuzi ya mwisho ni wewe
Usichukue nafasi ya haraka haraka kuwashirikisha ,marafiki zako bila kulichunguza tatizo lako na mpenzi wako, kaa angalia kama unaweza kulitatua tatizo ilo,chukua muda mrefu kujua sababu ya kutokea kwa kitu fulai hata kama ni cha furaha.na ikitokea umejikuta umeshasema kwa marafiki zao usiwafanye wakakuamulia cha kufanya.Sikiliza ushauri ila maamuzi ya mwisho yatoke ndani yako.
4.Jenga mawasiliano mazuri na mpenzi wako
Muda mwingine tunajikuta tunatangaza mahusiano yetu kwa sababu hatuna mawasilano mazuri na wapenzi wetu tulionao,jenga uhusiano mzuri wa kuwa wazi kwa mwenzi wako ili inapotokea jambo iwe rahisi kwenu kulizungumza na kutoa dukuduku.Ukishindwa kuongea na uliyenae ndio utajikuta utatafuta wa kumtolea dukuduku mtu wa nje.
5.Kubali kujifunza zaidi
Unapokuwa katika mahusiano unakutana watu wawili tofauti, kila mmoja anatabia yake, jitahidi kumsoma mwenzi wako ili kuelewa anataka nini na nini hapendi.Ukijifunza kumjua uliyenae haitakusumbua kuanza kutafuta ushauri kwa watu kwa sababu utajua nini cha kufanya linapotokea tatizo fulani.