Uongozi wa Ommy Dimpoz Wakanusha Taarifa Mbaya Kuhusu Msanii Wao
Uongozi wa msanii Ommy dimpozi umekanusha na kukemea vikali taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa msanii huyo alikuwa katika hali mbaya na kupatwa na umaauti kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Uongozi huo unasema kuwa taarifa hizo sio za kweli kwa sababu msanii wao mpaka sasa anaendelea poa na kwamba hali yake inazidi kuimraika na kubadilika siku hadi siku sio kama ile aliyokuwa nayo hapo awali.
Msanii huyo ambae aliwahi kuripotiwa zaidi ya mara moja kuwa mgonjwa sana, amekuwa akirudihswa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuangaliwa hali yake ingawa kuna kipindi aliwahi kuonekana kuwa imara zaidi kutokana na kuanza kuonekana katika mitandao ya kijamii.
Uongzio huo umewatoa wasiwasi mashabiki wa msanii huyo huku ukiwataka kuwa na maombi kwa ajuli ya msanii wao ili aweze kutoka katika majaribu hayo.