“Ugomvi Wangu na Ray C Utanipoteza”- Nandy
Mwanamuziki mkali wa Bongo fleva Nandy a.k.a The African Princess amefunguka na kukiri kuwa ugomvi wake namsanii mkongwe wa Bongo flva Rayc unaelekea kumpoteza.
Nandy na Rayc waliingia katika bifu zito mwaka Jana baada ya Nandy kutumia nyimbo za Rayc na kuziimba alipokuwa anatumbuiza katika tamasha la Fiesta jambo ambalo halikumfurahjsha Rayc na kulalama kuwa Nandy anaimba nyimbo zake wakati yeye mwenyewe yuko hai siyo vizuri.
Baada ya povu hill kumtoka Ray C alimpiga stop Nandy kuimba nyimbo zake zozote jambo lililosababisha kuwepo kwa hali isiyo shwari baina ya waremvo hawa wawili.
Baada ya kutoa wimbo mpya unaoitwa ‘Subalkheri Mpenzi’ alioshirikishwa na Aslay ambao kwa sasa unafanya vizuri na kushika chati mengine yamezuka kwani imesemekana kuwa Nandy amemuiga Rayc kwenye kuimba wimbo huo kuanzia sauti mpaka njia ya uimbaji alipopita.
Nandy amekana tuhuma hizo alipofanya interview na Enews ya East Africa TV na kufunguka yafuatayo:
Mimi sidhani kusema ukweli hebu wamsikilize Ray c na wasikilize na hii nyimbo sidhani kama zinafanana alafu hii nyimbo imeahafanyiwa kopi na msanii mwingine mwanamke ambye amekwisha fariki lakini pie kwenye suala la kurudia nyimbo mimi na Rayc tupo kwenye familia moja ya THT utaratibu wa kurudia nyimbo upo tangia siju nyingi na nimeukuta lakini yeye aliamua kunituhumu mimi kama namuibia nyimbo yake ingawa nilichukulia kawaida sana kwa sababu ulikuwa nimtazamo wake hata hivyo siwezi kufikiri sana itanipotezea umakini wangu”.