Umaarufu Wamponza Idris Sultan
Msanii wa maigizo ya vichekesho vya jukwaani Idris Sultan amefumguka na kusema kuwa tangu amekuwa na umaarufu sasa hivi watu wengi wamekuwa wakimchukulia kawaida sio kama alivyokuwa hapo awali alipokuwa mpiga picha.
Akiongea na Clouds Tv idris anasema kuwa kuna watu amekuwa akitamani sana kufanya nao kazi lakini wamekuwa wakimchukulia poa na kumuona kama hana umakini katika anachotaa kukifanya.
“kuna watu wamekuwa wakininyanyapaa sasa, hata wale wenye heshima zao , unakuta mtu unataka kufanya nae kazi lakini hakuoni kama kama huko sawa anakuwa anakuchukulia poa sana.
Idris anasema kuwa kuna muda amekuwa akiwaza labda asingekuwa maarufu angebaki kuwa mpiga pich ingsaidia kukaa na kufanya kazi na watu vizuri.