Umaarufu Haunipi Ninachokitaka :-Bright
Mwanamuziki Bright amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya sanaa na muziki amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kukosa gari hadi sasa ni kwa sababu amekuwa maarufu lakini hana kile anachokitafuta kwa muda wote.
Bright anasema kuwa umaarufu alioupata sio sawa na kile anachokipata kimslahi kitu ambacho kina vunja sana moyo wa kujituma na kufanya kazi.
Bright wa sasa sio wa mika ya nyuma, lakini pia umaarufu nilionao hauendani kabisa na kile nilichonacho, bado sijapata pesa kubwa hivyo ya ya kwamba ninaweza kununua hata gari.
Hata hivyo mwanamuziki huyo amegoma kabisa kuzungumzia uongozi wake wake wa Fundikila ingawa habari chini ya kaeti zinasema wawili hao kwa sasa hawaelewani.