Ukweli kuhusu biashara ya Wema kupigwa stop
Msanii Wema Isaack alikuja na biashara mpya ambayo wakidada wengi waliipenda kwa sababu ya uzuri wa bidhaa za mrembo huyo, Wema ambae aliaanza kwa kuzitambulisha lipstick zake zilizojulikana kama Kiss by Wema Sepetu zilipoingia kwa mara ya kwanza Tanzania wakidada walizigombania kama njugu sokoni hivyo bidhaa hiyo kuisha, shida imekuja katika kuendeleza bidhaa hizo kwa kuagiza mzigo mara ya pili ambapo kumekuwa na tetesi mbaya kuhusu bidhaa hizo.
Kumekuwa na tetesi kuwa biashara hiyo inaweza kufa kutokana na mzigo mpya ambao umeagiza umepigwa stop kisa tu bidhaaa hizo zinaonekana hazina ubora kama mwanzo.Tetesi hizo zinasema kuwa kutokana na kupendwa kwa lipstick izo sokoni ndio maana mzigo wa pili ulitengenezwa haraka bila kujali ubora wowote, na ni hatari kwa matumizi ya watu hivyo bidhaa hizo kukatazwa kuingia sokoni.
Lakini pia zipo tetesi kuwa inawezekana kuna watu wanaotaka kuchafua jina la msanii huyo kwa kusambaza tetesi hioz au kuingia mzigo fake kwa kutumia jina la Madame ili tu kumuharibia msanii jina.
Hata hivyo alipokuwa akitoa maelezo ya uwepo wa tetesi hizo katika kituo cha EATV , meneja mpya wa Madame Wema Sepetu aliejulikana kwa jina la Happy Shame amesema mzigo huo haupo sokoni kwa sasa kwasababu msimu wa kuangiza mzigo mpya bado na sio kweli kwamba mzigo umezuia kwa sababu hauna ubora .
“Hicho kitu sijakisikia na wala sijatumia katika email yangu kwamba lipstick zimezuiwa . Hivi vitu vinaenda na msimu , muda wake ukifika tutaziachia kwaiyo hakuna ukweli isipokuwa kuna baadhi ya vitu tunavikamilisha baadae mzigo utatoka” anasema Happy Shame.
Hivyo basi uwepo wa tetesi za kusimamishwa kwa bidhaa za lipstick za Wema Sepetu zinaweza kuwa si za kweli ilhali meneja wa msanii huyo amethibitisha kuja kwa bidhaa hizo endapo taratibu za uingizaji wa bidhaa hizo nchi utakamilika, hivyo kwa wateja waliokuwa wanasubiri bidhaa hizo wanaweza kutokwa na wasiwasi kwa kusikiliza pia maneno ya meneja.