Ukaribu Wa Petit Man na Lynn Wazua Gumzo Ukumbini
Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva na ambaye pia ni meneja wa wasanii wengi Hamad Manungwa ‘Petit Man’ na mrembo Irene Hillary maarufu kama Lynn wamezua gumzo kutokana na ukaribu wao.
Global Publishers wanaripoti kuwa wawili hao waluonekana pamoja ndani ya Klabu ya Next Door Arena iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mwanamuziki, Faustina Charles ‘Nandy’ alikuwa akisheherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ samba mba na kuzindua albamu yake iitwayo African Princes.
Wawili hao wakiwa ukumbini hapo walionekana kuwa na kikao kizito na pozi lao kuzua mino ng’ono ndipo walipofuatwa na GPL, ili kujua walicho kuwa wakijadiliana ambapo Petit Man alisema wako kwenye mikakati ya kikazi.
Usione tuko kwenye pozi hili na tunano ng’onezana ni kwamba kuna kitu tunaandaa na Lynn na muda si mrefu tunataka kufanya bonge la sapraiz kwa mashabiki wa burudani hivyo watu wasitufikirie vibaya“.
Ukaribu wao ukimya gumzo kutokana na kwamba Petit alikuwa mume wa Esma Dada yake na Diamond na Lynn alikuwa Mpenzi wa Diamond Platnumz.