Ujumbe wa Dogo Janja kwa Nandy
Baada ya drama zote kutokea katika mitandao ya kijamii kwa siku hizi mbili mfululizo kwa msanii wa kike Nandy hasa baada ya kuvuja kwa picha akiwa na mpezni wake Billnass wakiwa faragha, msanii mwenzake Dogo janja amejaribu kumtia moyo kwa yote yaliyotokea.
Dogo janja ambae ameshafanya kazi na nandy pia ameonekana kuguswa na tukio hilo lakini zadi ameonekana kuumia kwa jinsi nandy alivyofunguka na kumba msamaha kitu kinachoonyesha kuwa ameumizwa na matukio hayo.
Katika ukurasa wake wa instagram dogo janja aliandika’asiyekuchoka kwenye shida Mungu atamlinda zaidi ili mcheke wote kweny raha #myrichfriend @officialnandy’