Uchebe: Bora Kufa Kuliko Kumkosa Shilole
Uchebe Ashraf ambaye ni mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo fleva, Shilole Kiuno amefunguka na kudai ni bora afe kuliko kuishi maisha yake bila kuwa na mpenzi wake Shilole.
Wiki iliyopita kuna habari zilienea na zikisindikizwa na picha iliyomuonyesha Shilole na mpenzi wake wa zamani Nuhu Mziwanda wakiwa kitandani wamelala kimahaba kabisa huku habari zikidai kuwa Shilole kamwaga mchumba ake Uchebe na kumrudia Nuh Mziwanda.
Lakini mara tu habari hizo zilivyoanza kuenea Shilole alitumia mitandao ya kijamii kukana taarifa hizo na kuweka wazi kuwa ile picha iliyokuwa inasambaa mtandaoni ilikuwa ni picha ya zamani enzi yupo na Nuh na aliyesambaza picha hizo ni Nuh katika jitihada zake za kutaka kumgombanisha na Uchebe, tuhuma ambazo Nuh alizikataa kupita kiasi.
Baada ya sakata hilo Mpenzi wa Shilole, Uchebe aliweka wazi kuwa taarifa hizo zilikuwa za kweli lakini pamoja na hayo kuliko kumuacha Shilole basi bora afe tu. Kwenye mahojiano aliyofanya na Over The Weekiend Uchebe amekiri kuwa pamoja na kuwa amegundua kuwa Shilole alirudisha penzi lake kwa bwana ake wa zamani Nuh Mziwanda lakini hayuko tayari kumuacha:
Najua Shilole amenikosea sana lakini siko radhi kumuacha ninampenda mno na niko radhi kupoteza maisha yangu kwa ajili yake au niuze chochote nilichonacho ilimradi tu nimridhishe kwa chochote atakacho yeye”.