Tunda Apania Kurudi Shule Kujiendeleza Kielimu
Video vixen maarufu asiyeisha vituko kwenye mitandao ya kijamii Anna Sebastian Kimario ‘Tunda’ ameweka wazi mipango yake ya kutaka kurudi shule kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Tunda amesema kuwa, lengo lake ni kuwa mtaalam wa mambo ya kompyuta hivyo anataka akasomee kozi ya Information Technology (IT).
Siku zote napenda kusomea kozi ya IT, ni kitu kilichopo kwenye ndoto yangu na kwa sababu sasa nimekua na kutulia, naamini nitasoma kwa utulivu kabisa“.
Tunda amekiri kuwa pamoja na kupoteza muda mwingi kufanya mambo ambayo amekuja kugundua kuwa hayana faida kwake kiasi hicho ameamua kutopoteza muda zaidi na kurudi shuleni kwani muda inamruhusu bado.