Tunda Amuombea Amber Rutty
Mwanadada ambae amekuwa na jina kubwa kutoka ana kazi yake ya kuwa video vixen katika video za wasanii mbalimbali , TUNDA , amefunguka na kusema kuwa wa sasa amekuwa muoga sana wa kufanya kitu chochote .
Tunda anasema kuwa anawaombea sana watu wanaofanya hivyo kwa sababu hawajui lile walitendalo lakini pia anaomba hata Mungu awaongoze ili wasitake kurudia tena , na kwa upande wa Amber Rutty anasema hawezi kumsema kitu lakini anaamini kuwa mwanadada huyo kwa sasa atakuwa akipitia katika wakati mgumu.
Tunda anasema kuwa kwa sheria kali zilizopo sasa hii nchini inakuwa kazi sana hata kwake kufanya vitu anavyoviita yeye kuwa ni vya kipumbavu kwa sababu anaogopa hajui nini kinaweza kumpata .
Kama inakumbukwa , tunda aliwahi kuvujisha pia picha na video akiwa faragha na moja ya vigogo nchini lakini alijitokeza yeye na mhuiska na kuomba msamaha na tangu hapo mwanadada huyo anasema kuwa amejifunza sana.