Tunda Amuomba Radhi Mke wa Kinje Baada ya Video Zake na Kinje Kuvuja Mtandaoni (video)
Mrembo Tunda ametawala vichwa vya habari sana kuanzia wiki chache zilizopita kutokana na skendo ya kutembea na Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mpaka Jana kuingia kwenye vita ya maneno na Aunty Ezekiel.
Baada ya kugombana na Aunty Ezekiel kuhusu pesa anayodaiwa baada ya kukopa chupa ya pombe ya belaire, Tunda ameingia tena kwenye skendo nyingine ya kutembea na mume wa mtu.
Siku ya jana video kadhaa zilisambaa mtandaoni zikimuonyesha akiwa analiwa denda na mmoja wa matajiri wakubwa Tanzania Kinje. Kinje ni maarufu kwa sababu ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe Kinjekitile Ngwale. Kinje ni mfanyabiashara maarufu kwa muda mrefu amesemekana kuwa ni sponsa wa TundaTunda.
Baada ya video hizo kusambaa watu wengi walishangazwa kwani Kinje ameoa ni mume wa mtu na ana watoto watatu na mkewe anayeitwa Anita, lakini pia watu wengi walionekana kushangazwa has a kutokana na tofauti kubwa waliyokuwa nayo kiumri kwani Tunda ni mtoto mdogo sana wa miaka ishirini na Kinje baba mtu mzima sana.
Hizi ni baadhi ya video zinazomwonyeaha Tunda akifanya yake na sponsa wake Kinje:
Baada ya sakata hilo Tunda alichukua muda wake na kuandika ujumbe wa kumuomba radhi mke wa Kinje lakini pia alimwaomba radhi mashabiki zake wote kwa kusambaa kwa video zile.