Tunda akanusha tetesi za kutoa ujauzito
Yule mwanadada anaetikisa jijini Dar Es Salaam hasa katika upande yeye wa kuwa moja kati ya video vixen bora na amekuwa akionekana katika video nyingi za mastaa wakubwa nchi , Tunda Sebasita anafahamika kwa jina la umaarufu kama Tunda leo amefunguka na kukanusha stori zilikuwa zikisambaa katika mitandao kuwa alikuwa mjamzito kipindi cha nyuma na sasa ameitoa mimba iyo, hata hivyo kuenea kwa tetesi izo kunasababishwa na mrembo huyo (Tunda) ambae amekuwa akipost picha huku akionyesha sehemu za tumbo lake ambapo watu walianza kujudge na kusema kubwa mrembo huyo atakuwa ni mjamzito, lakini bado hata muda ulipopita bila kuona maendeleo yoyote basi tetesi zilibadilika na kusemekana kuwa ametoa mimba iyo.
Hata hivyo Tunda amekanusha tuhuma hizo zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa kwa upande wake taarifa hizo ni ngeni, na wala hakuwa na mimba na katika maisha yake hajawahi kupata mimba kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari wa kituo cha EATV, Tunda anasema kuwa sababu za yeye kuwa na tumbo ni kitambi tu kilichokuwa kinakuwa sababu ya yeye kunenenpa maana yaye ana asili ya tumbo ila kwa sasa anafanya diet na ndio maana watu wanaona tumbo linaisha.
“Sina mimba na sijawahi kupata ujauzito hilo tumbo limeongezeka tu nina asili ya tumbo nikinenepa na tumbo linaongezela hizo tetesi za kutoa mimba ndo nazisikia kwako sijawahi kupata wala kutoa mimba kabisa.”
Tunda ni moja ya video vixen maarufu hapa nchi na amekuwa akitokea katika video za wasanii wakubwa maarufu nchi.baaadhi ya video zake ambazo ameshawahi kutokea ni pamoja na “Salome” ya Diamond Platinumz, pamoja na “Furaha” wa Young Dee
Tunda ni mmoja kati ya video queen mwenye drama nyingi sana za kwenye mitandao kutokana na picha anazoposti katika ukurasa wake wa instagram, na katika historia yake mrembo huyo alishawahi kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva Young Dee mwenye kibao kipya cha “Utani utani”