Tunda Abambwa na Diamond Baada Ya Kumwaga Casto (+video)
Socialite na video queen maarufu Bongo Tunda Sebastian amerudi Kwenye headlines baada ya kuonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Tunda ameshawahi kusemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond lakini baadae alianzisha Mahusiano na Mtangazaji wa clouds Tv Casto Dickson.
Pamoja na kwamba Casto alichora bonge la Tattoo ya Jina la Tunda Kwenye Mkono wake lakini aliishia wiki chache zilizopita na siku ya jana ameonekana Kwenye Birthday party Diamond.
Diamond alionekana akicheza na Tunda kwa ukaribu sana kiasi ya kupelekea kuzua tetesi za kuwa Tunda kamtosa Casto na Kurudisha majeshi yake kwa Diamond.
https://www.instagram.com/p/BodZvdkn_6e/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1mcmagtlbnvu
Siku ya jana ilikuwa ni Birthday party ya Diamond na housewarming party ya nyumba yake mpya ambapo alifanya Private party na kualika Mastaa kibao ikiwemo timu nzima ya WCB , Navy Kenzo, Dully Sykes, Billnas, Tunda na wengineo.