Tulipanga na Vannesa Nikae Big Brother Wiki 2 Tu: Feza Kessy
Msanii wa kike amabe pia ni mtangazaji wa Times Fm, Feza Kessy amefunguka na kusema kuwa lengo lake kubwa la kwenda katika mshindano ya big brother mwaka 2013 ilikuwa ni kw ajili ya yeye kujulikana kwa sababu aliamini kuwa endapo atakaa hata muda kidogo tu jina lake litakuwa na kuanza kuuza muziki wake.
Kama ambavyo alishawahi kusema kuwa yeye na Vannesa ni washkaji sana, Feza Kessy anasema kuwa hakuwahi kuangalia Big Brother kabla lakini kutokana na msukumo mkubwa aliokuwa ameuata kutoka kwa vannesa mdee kuwa anaweza kufanya hivyo basi aliona isiwe shida, Feza anasema kuwa Vannesa ndio alimletea hadi fomu za kujaza kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.
sikuwahi kuangalia big brother kabla ya hapo na mara ya kwanza nilivyoenda nilikosa kwa sababu ilikuwa ni ya couples,lakini vannesa aliniambia feza you can do this we nenda.
nilikuwa nawaza jinsi gani muziki wangu unaweza kuuza mapema, kwenda big brother ilikuwa ni marjkrting strategy yetu,vee aliniambia nikakae tu hata wiki mbili zinanitosha nikitoka huko ninakuwa feza wa big brother, feza wa big brother inakuwa poa, lakini sikujua kama ningeweza kukaa hadi the last week.Vee na Abby ndio walinipeleka mpka kwenye audition siku naenda airpot gari la abby ndio lilitumika kunipeleka .
Ni kwamba watu hawajui tu lakini muziki unahitaji background yako, mimi watu wanashangaa imekuwa mpaka ametusua hivi lakini kiukweli kabisa nilianza muziki before hiyo 2013 lakini sikuwa nafanya vizuri lakini niliona kabisa BBA ingenipa platform.
Feza kesy ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha simple alikuwa mshiriki wa big brother kutokea tanzania akiwa na nando ambae aliwahi kutolewa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha ndani ya jumba hilo.Feza Kessy anakiri kuwa mashindano hayo yamempa background nzuri ya kimuziki wake wa sasa.