Tin White Awaponda JB na Wema Sepetu.
Mchekeshaji maarufu bongo Tin White ameibuka na kumchana wema sepetu pamoja na JB kwamba sio wasaniiwa ukweli ila washukuru mungu kwa kufika hapo walipo sasa kutokana mitandao ya kijamii mbayo imekuwa ikiwakuzia majina yao.
Tin White ameongea hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNews,baada ya kuwepo kwa wimbi la wasaini wengi kwa sasa ambao wamekuwa wakiingia katika sanaa bila kupitia vyuo vinavyohusiana na sanaa hivyo wamekuwa wakiharibu tasnia hii ya sanaa.
Unajua kuna kipaji yaani hiyo ni reality kabisa lakini pia kuna muongezo wakina kanumba walikuwa wanafanya kwa vipaji vyao vyenyewe tu lakini hawa wakina wema sepetu walikuja tu kujaribu hao sasa ndo wa kuongezea .
mimi naongea ukweli kabisa kutokana na mitandao ndo maana wakina Wema Sepetu wameweza kuitika lakini hana reality yoyote ile.Hata huyo JB hakwa na historia ya kuwa msanii alikuwa anauza mahindi ila yeye alilazimishwa na Single Mtambalike ili awe msanii siongei kwa ubaya ila naongea jambo la ukweli kabisa.