Tazama Jinsi Zari Alivyofanya Birthday Party Ya Kifahari Uganda
Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ambaye ni mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefanya party la kifahari nchini Uganda.
Zari ambaye alisheherekea Birthday yake tarehe 23 Sepetemba lakini aliungana na Familia yake inayoishi nchini Uganda kwa ajili ya Kusheherekea na ndugu zake na marafiki.
Sherehe hiyo iliyofanyika katika hoteli ya kifahari ilihudhuriwa na marafiki na ndugu kadhaa wachache ambapo watu maarufu walikuwa ni pamoja na Captain Mike Mukula, dada wa Zari, Aly Alibhai na mkewe, Sylvia Wilson Namutebi.