Baada ya Uokovu,Tatoo Zinamtesa Munalove .
Msanii wa maigizo nchi, Muna Love amekiri kuwa tatoo alizochora mwilini mwake kipindi hajaokoka zimeanza kumtesa kwa sababu hata mtoto wake wa kiume amekuwa akimpigia kelele kila siku kuhusu kuziondoa tatoo hizo.
Muna ambae mara ya kwanza alikuwa katika mambo ya kidunia na baadae alipata matatizo makubwa yeye na mwanae yaliyoyafanya kuokoka na kumrudia mungu, anasema kuwa anatamani kuzifuta tatoo hizo na kuondoa kabisa.
Mtoto wa kiume wa Muna ambae pia ameokoka amekuwa akimsumbua mama yake huyo kuzifuta tatoo hizo kwani zinaenda kinyume na maadili ya uokovu.
Muna akiwa na mtoto wake.