Tanzia: Msanii Oliver Mtukudzi Afariki Dunia
Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia. Amefariki hii leo katika hospitali ya Avenues mjini Harare. Mtukudzi amekuwa akiugua kwa muda sasa.
Kwa mujibu wa BBC,Alilazimika kukatiza miadi kadhaa katika fani hiyo ya muziki katika mataifa mbali mbali duniani kutokana na kuugua kwake.
Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith.
Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa anapewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii kama Hugh Masekela, Steve Dyer, Miriam Makeba, Yousssou N dour, Angelique Kidjo, Yvonne Chaka Chaka na Lady Smith Black Mambazo.