Tanasha Awatumia Ujumbe Huu Maadui Zake
Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu ambao wamekuwa wakimfanyia ubaya.
Tangu Diamond na Tanasha waweke wazi mahusiano yao wiki chache zilizopita mrembo huyo amekuwa akilalamika na watu ambao wamekuwa wakimponda kila kukicha.
Wiki iliyopita tu Tanasha aliwatolea Povu zito watu ambao walikuwa wanamponda shepu yake na kudai ana shepu mbaya na miguu mibaya ambapo alisema hata Kama mbaya ndio hivyo Diamond ameshampenda na atamuoa.
Siku ya jana tena Tanasha aliwatolea Povu mashabiki wa Instagram ambapo aliwatumia ujumbe wabaya wake kuwataka kuwa wavumilivu kwani kuna mengi makubwa anakuja nayo ambayo yatazidi kuwakera.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha aliandika: